May 13, 2019


MAJINA ya wachezaji watatu mafundi wa kupachika mabao Ligi Kuu England yameleta hisia ya furaha kwa nyota hao ambao wameshinda viatu cha dhahabu kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu England na kudhihirisha kwamba ni mashine za magoli.
Washambuliaji watatu ambapo wawili wa Liverpool ambao ni Mohamed Salah anayetokea Misri na Sadio Mane mchezaji wa timu ya Taifa ya Senegal pamoja na Pierre Aubameyang anayekipiga timu ya Taifa ya Gabon.
Wote watatu wameshinda vita ya ufungaji bora msimu huu baada ya kufunga jumla ya mabao 22 kwenye Ligi hiyo ambayo jana ilihitimisha mbio zake na bingwa kuwa ni Manchester City.
Kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burney ambapo Abemayang alitupia mawili ilimfanya amfikie Salah pamoja na Sadio Mane ambaye naye alifunga mabao 2 kenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolves.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic