May 13, 2019


MENEJA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa hajafurahishwa na uwezo ambao wameonyesha wachezaji wake kwenye mchezo wake wa mwisho kwa kuwa walicheza chini ya kiwango na kuruhusu kufungwa mabao 2-0 na Cardiff.
Manchester United wamemaliza Ligi Kuu England wakiwa nafasi ya sita baada ya kucheza michezo 38 wakiwa wamejikusanyia pointi 66.
"Hatukuwa kwenye ubora wetu, wachezaji wamecheza chini ya kiwango, tumemaliza msimu tukiwa na nguvu kidogo kwa ajili ya msimu ujao.
"Tulikuwa na nafasi ya kumaliza tukiwa ndani ya nne bora, ila michezo yetu miwili ya mwisho tuliboroga na imetugharimu tufike hapa tulipo, kiukweli michezo yetu yote ya mwisho sina uhakika kama tulionyesha juhudi.
"Tulitakiwa tushinde mchezo wetu dhidi ya Huddersfield ila tukalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 hapo ndipo makosa yalianzia hapo, ligi ni ngumu na haijalishi unacheza na nani ni lazima upambane," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic