May 24, 2019


MENEJA Mauricio Pochettino ameshashiwa kubaki ndani ya kikosi cha Tottenham na kusema kuwa ni miongoni mwa timu bora ambayo inashiriki ligi bora duniani.
Pochettino alinukuliwa akisema kwamba mchezo wake wa mwisho utakuwa dhidi ya Liverpool ambao utakuwa ni wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo kama wasingemsajili mchezaji mmoja kwa gharama kubwa kwenye dirisha la usajili angebwaga manyanga.
Hata hivyo ametengua kauli yake hiyo kwa kuwa bado anaona timu hiyo ya Spurs ina maono makubwa na kuelezea namna anavyoiona ikiwa ni miongoni mwa timu bora duniani.
"Leo Tottenham ni kwa ajili yangu, ni klabu bora ndani ya ulimwengu wa michezo hasa ukizungumzia upande wa miundombinu, maeneo ya kujifunzia uwanja mzuri ambao ni bora hakuna klabu bora kama hii.
"Pia ndani ya Uingereza hakuna mji mzuri zaidi ya England, na ligi bora duniani ni ligi kuu ya England na ni ngumu pia miongoni mwa ligi ambazo zimewahi kutokea, hivyo malengo yangu ni kuifanya Totthenham kuwa timu bora duniani," amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic