May 24, 2019

KOCHA Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake watatu kikosi cha kwanza hawataonekana kwenye kikosi chake mpaka msimu ujao kwani kwa sasa hali zao bado sio fiti.

Aussems ambaye amekiongoza kikosi cha Simba msimu huu kutwaa ubingwa kikiwa na pointi 91 huku kikiwa na michezo miwili amesema kuwa nyota hao watasubiri mpaka msimu ujao.

"Paul Bukaba, Shomari Kapombe pamoja na Asante Kwasi hawa bado hawajatengamaa kwa msimu huu sitakuwa nao kwenye kikosi changu mpaka msimu ujao.

"Najua kwamba kila mchezaji ana umuhimu wake hivyo nitawatumia wengine kuziba nafasi zao ili nipate matokeo kwenye michezo iliyobaki kwani hakuna kocha ambaye anaingia uwanjani akifikiria kushindwa," amesema Aussems.

Michezo iliyobaki kwa Simba ni dhidi ya Biashara United utakaochezwa kesho uwanja wa Taifa kabla ya ule wa kumalizia msimu dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa uwanja wa Jamhuri, Mei 28.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic