May 21, 2019


ANGEL Eaton, mchezaji wa mchezo wa Golf Tanzania amesema kuwa haikuwa rahisi kwake kupata tuzo 34 na kuongezewa nyingine ya heshima na gazeti la Championi leo alipotembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori.

Angel ambaye anachezea timu ya Lugalo amesema kuwa tatizo kubwa ambalo linamkwamisha kufikia mafaniko makubwa ni kutokuwa na mdhamini kutokana na mchezo wa Golf kutumia vifaa vingi vya gharama ambavyo ni lazima kuwa navyo.

“Mchezo wa Golf ni kipaji changu ila imekuwa ngumu kufikia mafanikio zaidi ya hapa nilipo kutokana na gharama za kuendesha mchezo huu, ila kwa hatua ambayo nimefikia ni kutokana na juhudi na kukubali kile ambacho ninakifanya.

"Ilichukua mwaka mzima kuuelewa vizuri mchezo, na hapo sio kupiga mipira kumi, unatakiwa angalau upige mipira 500 kwa siku, kwa hiyo haikuwa kazi rahisi,ila ninashukuru kwa sapoti ambayo nimekuwa napata hata kwa ajili ya tuzo ya heshima ambayo nimepewa leo na gazeti la Championi ni jambo la faraja nitaendelea kupeperusha Bendera kimataifa kila siku” amesema.

Tuzo hizo 34 ambazo ameshinda katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ni pamoja na Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic