May 21, 2019


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amemwambia nahodha na mshambuliaji wa klabu hiyo Ibrahim Ajibu kufikilia mara mbili kuhusu kuihama klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Imeelezwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Zahera amedai Ajibu ni kiongozi wa wenzake na hapaswi kuwa na mawazo ya kuondoka Yanga na kuwaacha wenzake.

Imeendelea kusema kuwa mkataba wa Ajibu na Yanga unaisha mwisho wa msimu huu na inadaiwa kuwa atajiunga na klabu ya Simba baada ya mkataba wake kuisha na Yanga.

Taarifa za Ajibu kuondoka Yanga zimeanza muda mrefu uliopita na kuleta sintofahamu kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokana na namna mwendendo wa klabu ulivyo.

Zahera amemuomba Ajibu afikirie zaidi ya mara moja kuhusiana na kuondoka kwake kwa manufaa ya Yanga maana anaheshimu mchango wake.

5 COMMENTS:

  1. Anajaribu kumghilibu Ajibu mwenye akili zake timamu. Ana vituko vya hali ya juu. Ajibu eti afikiri vizuri kutaka kwake kurejea Kule kwao alipozaliwa, kutunzwa na kukulia eti asije akajuta kupoteza pepo. Ajibu anataka kujinasuwa nawe unataka kumkomalia kuendelea kuishi maisha yasiyokuwa na dhamana ya kila aina ya migomo. Mwachie mtoto wawatu arejee Kwa wazazi wake Kwa Salama na Amani mwache atazame maslahi yake huyo keshachoka na ugumu WA maisha kama alivo Kakolanya

    ReplyDelete
  2. Kuna mchezaji kipenzi Yanga kama makambo na Zahera ndie aliekuwa mpambe au wakala wa kumtafutia mkongo mwezake timu bora zaidi ili aweze kucheza klabu bingwa Africa. Kama kweli Simba wanamuhitaji Ajibu basi akiacha nafasi atakuwa mgonjwa wa akili kwani licha ya uwezekano wa kupata nafasi ya kucheza klabu bingwa Africa na kuonesha uwezo wake lakini atakuwa na uhakika wa mshahara wake wa mwezi.Mechi kama hii ya sevila na Simba ilikuwa nafasi yake pia Ajibu kuonesha uwezo wake sijui ni nani aliemshauri Ajibu kwenda Yanga?

    ReplyDelete
  3. Si wakati ule anbapo Yanga wakijivunia hela ya Manji na uhaba WA mishahara ya Hakika hivi sasa na kunona Kwa mnyama ndipo kulipomuamsha Ajibu mapema

    ReplyDelete
  4. Hv jaman huyu zahera yeye akili yake huwa inapoteza mawasiliano au kuna nn?. Mimi binafsi najiuliza kuwa Makambo alikuwa n mtu muhimu sana pale Yanga na kiukweli angekuwa na viungo kama wa Simba jamaa angekuwa mbali sana kwa magoli sio siri. Lakin huyuhuyu Zahera kadanganya kama kawaida yake et anaenda kuangalia mafamilia kumbe ndo anampeleka Makambo Guinea, badala ya kumtafutia makambo viungo na wachezaji wa kuweza kuboresha safu ya ushambuliaji ya yanga yeye ndo anaibomoa kwa ajili ya maslahi lakin huyuhuyu zahera anasema Naipenda sana Yanga hapo tuangalie kuna upendo gani hapo?. Uunadhani kama makambo angetafutiwa wachezaji wazuri hapo mbele kungekuwa na nini? baadae?. Sasa yeye anamshawishi Ajibu kubaki yanga kwa hela za kuchangisha ni kweli? usajili bilion mbili. sasa baadae maisha yataendaje au tena tutarudi kuchangisha. Zahera anatupoteza kwa maslahio yake sisi tukimsujudi tutakumbuka shuka kumekucha, Ajibu na wewe angalia maisha yako ya baadae pamoja na familia yako kwan maisha ya mpira ni miaka michache sana piga fedha za MO uangalie mengine baadae wakati ndo huu.

    ReplyDelete
  5. Uongozi mpya yaani umekuja na nuksi....wale Wanayanga wenye hasira wako wapi? Habari zinaendelea kuwa si nzuri sana wachezaji wote tegemeo wanaondoka wengine wakiuzwa na wengine mikataba ikiisha bila kuongezwa....jamani jamani hebu harakisheni kuokoa hali.....maumivu yanaendelea....hakuna habari njema wiki hizi mbili na mwezi mzima wa 5. Rekebisheni hali kwa kusajili at least mikataba ya awali ili kutoa moyo na kutia hamasa kwa wapenzi kuendelea kuchangia.....ukimya huu unaogopesha na ni hatari....mmeshaijenga chuki kwa wanayanga kuna wadau wa Yanga hawajitokezi kusaidia kwa kuwa tu hakuna dalili za kuanza kuleta mashine za uhakika hakuna hata mikataba ya awali kwa washambuliaji wakali na viungo wakali au mabeki wakali....Kuna kundi kubwa limeandaa fujo hawa ni wanachama ambao hawapendi hizi habari za huzuni zinazoendelea (Ajibu anaondoka burr, Makambo anauzwa, wachezaji 7 wanaumwa kuikosa Mbeya City, ubingwa kuchukuliwa na Simba, Sportspesa kuileta Sevila kucheza na Simba na siyo Yanga...nk. Na habari mbaya ndio zinazoendelea) Sasa amani ya nchi itavurugika....kwa kuwa kuna watu wanaumizwa na hizi habari...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic