May 5, 2019


MTOTO wa marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye anawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, amesema akipata nafasi hiyo, kwa kushirikiana na viongozi wengine, atahakikisha timu yao haishindwi ‘upande wa pili.’

Akizungumza wakati wa kampeni zake, Maalim Hassan, alisema ametambua kwamba Yanga wanahitaji mjumbe ambaye ni rahisi kufikiwa na wanachama ili kutoa ushauri, hivyo amejitathmini na kujiona yeye anafaa kuvaa viatu hivyo.

Aliongeza kuwa, pia Yanga inahitaji mjumbe mbunifu ili klabu iwe inafanikiwa, katika yote hayo, yeye yupo tayari kuhakikisha mabadiliko yanakuwepo ndani ya klabu hiyo ili iendane na wakati uliopo.

“Kwa kushirikiana na viongozi wengine watakaochaguliwa, nitahakikisha kunakuwa na ukweli na uwazi katika masuala ya fedha ili timu ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Tutabuni mikakati endelevu na kushauri namna bora ya kuisimamia klabu ikiwa ni pamoja na miundombinu na tutaanzisha timu za vijana wa umri mbalimbali,” alisema Maalim Hassan.

Ikumbukwe kuwa, Jumapili hii Yanga itafanya uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi watakaoingia madarakani kwa kipindi cha miaka minne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic