May 5, 2019


UONGOZI wa Simba umefunguka kuwa, malengo yao ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara wakiwa bado na mechi mkononi na siyo kusubiri mpaka mechi ya mwisho, ndiyo maana hawafanyi makosa wanapopata nafasi.

Simba hadi sasa imecheza mechi 29 na kusaliwa na mechi 9.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Katibu wa Simba, Dk Arnold Kashembe, alisema lengo ni kutangaza ubingwa kwa kushinda kila mechi iliyopo mbele yao.

“Mipango yetu kama klabu ni kuona Simba inatwaa ubingwa mapema, hatutaki kusubiri mpaka mechi ya mwisho wa ligi, hapana, tunatwaa ubingwa na mechi zetu mkononi.

“Ndiyo maana tunapambana kuona tunashinda kila mechi ambayo iko mbele yetu, kama hivi timu inaenda Mbeya, mipango ni kurudi na pointi sita muhimu, kwa sasa hakuna cha kupoteza.

“Tunataka kutetea ubingwa wetu mapema, tukiwa na tiketi ya uhakika mkononi kwa ajili ya michuano ya kimataifa mwakani, jambo ambalo ndiyo ndoto yetu na kufanya vizuri.

“Na hapa tulipofika wapinzani wetu hadi sasa kwenye msimamo ni Yanga, hivyo ushindi kwa kila mechi ndiyo utakaotubeba sisi,” alisema Kashembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic