May 21, 2019


ETTIENE Ndayiragije Kocha Mkuu wa KMC leo ameiadhibu timu yake ya zamani Mbao FC kwa kuifunga mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa CCM kirumba.

Kabla ya kujiunga na KMC, Ndiyaragije alikuwa Kocha Mkuu wa Mbao FC.

Mabao ya KMC yalifungwa na Babilas Chitembe dakika ya pili ambaye alijifunga  na bao la pili lilifungwa na George Sangija dakika ya 39.

Ushindi hu unaifanya Mbao ambayo imecheza jumla ya michezo 37 kubakiwa na mchezo mmoja mkononi ili kukamilisha mzunguko wa pili huku ikiwa na pointi 44 na wapinzani wao KMC kuwa nafasi ya nne baada ya kucheza mihezo 37 wakijikusanyia jumla ya pointi 52.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic