May 13, 2019


KESHO uwanja wa Uhuru, kikosi cha Yanga kitamenyana na Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa majira ya saa 10:00 jioni.

Nyota watatu wa Yanga wataukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten hawa hapa:-

Mohamed Banka, Gadiel Michael na Andrew Chikupe.

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 80 endapo watashinda mchezo wa kesho watarejea kwenye nafasi yao.

2 COMMENTS:

  1. Huyu Kocha ndio maana anatakiwa asimamiwe na asiwafanye Yanga wote ni wajinga haiwezekani atamke kuwa eti atasajili wachezaji 8 tu....hata asiye na akili na soka anaelewa kuwa Yanga imekuwa dhaifu mno na zaidi ya 3/4 ya wachezaji waliopo kikosini hawafai hata kuendelea kubaki Yanga....sasa atakujaje na kusema atasajili wachezaji 8 tu? Ndio maana wanayanga wanahamasishwa kuchangia na kukusanya fedha ili waunde timu imara na kusajili wachezaji bora wa kutosha waondokane na hali iliyopo...tatizo halitakuwa pesa tena kwani watakuwa na fedha ya kutosha kusajili na kulipa mishahara....asiwafanye wanayanga warudi kule walipotoka kwa kuwa na kikosi dhaifu chenye wachezaji wa nje na ndani ya nchi ambao wengi wao ni magarasa wa kiwango cha chini ambao hata wakicheza na Lipuli, Ndanda, Singida United wanafikiria "kupaki basi". Yanga wanataka wachezaji wa kiwango cha juu mno wakushindana na kutoa upinzani wa hali ya buy kwa timu kama Simba, TP Mazembe, Al Ahly nk...hata kama hawata shiriki mashindano ya CAF lakini wataisaidia kuchukua ubingwa wa ligi hayo ndio matamanio na mahitaji yao wapenzi na wakereketwa wa Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic