May 13, 2019


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wamebanwa mbavu na mabingwa wa Afrika Masharika na kati Azam FC kwenye mchezo uliochezwa leo uwanja wa Uhuru.

Simba ambao leo walikuwa wenyeji, mchezo wa kwanza waliifunga Azam FC mabao 3-1 uwanja wa Taifa, lakini leo mambo yamekuwa magumu na kukubali kutoshana nguvu kwa timu zote kushindwa kuonyeshana ubabe.

Azam nao leo wameshindwa kulipa kisasi kwa kuitungua Simba mabao 3-0 kutokana na ushindani uliokuwepo.

Sasa Simba wanaongezewa mlima wa kuzitafuta pointi nane zilizobaki ili kutetea ubingwa wao msimu huu.

Azam FC wao wanasalia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 69 na wamesaliwa na michezo miwili ili kukamilisha mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Simba wanabaki nafasi ya kwanza baada ya kucheza michezo 33 wamejikusanyia pointi 82 huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya pili na wana pointi 80 wamebakiwa na michezo mitatu mkononi.

3 COMMENTS:

  1. Azam anashangilia sare duuh skutegemea hill timu kama azam kushangilia sare

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa ulitaka walie, mbona simba alishangilia sare na mtibwa msimu uliopita

      Delete
    2. wacha uongo wa mchana

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic