May 5, 2019



WASHAMBULIAJI wa Simba ambao wanaunda safu ya ushambuliaji yenye mabao mengi mpaka sasa, wanadaiwa mabao 6 tu kuvunja rekodi iliyowekwa na ile pacha ya Yanga msimu wa mwaka 2015/16.
Msimu wa 2015/16 safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyokuwa inaundwa na Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Simon msuva wao walifunga jumla ya mabao 47.
Tayari safu ya Simba inayoongozwa na Kagere imeshafunga jumla ya mabao 41 tofauti ya mabao sita tu kuvunja rekodi iliyowekwa na safu ya Yanga ambayo mpaka sasa haijawahi kufikiwa na pacha yoyote bongo.
Simba wamebakiwa na michezo nane kukamilisha Ligi Kuu Bara, hivyo kama watatumia nafasi zao vizuri huenda wakaifikia rekodi hii.

1 COMMENTS:

  1. tuachane na 2015/2016! Hadi sasa msimu hus Simba inamdai Yanga mabao mangapi?
    labda tukumbushane...SImba ikiwa bado na viporo 5, inaidai Yanga bao 6 za kufunga, na imefungwa nusu ya mabao 24 ambayo tayari Yanga wametunguliwa!
    Namna mambo yanavyoenda hayo mabao 6 ya 2015/2016 yatarudiswa maradufu!
    Halafu haiingii akilini pale unamsikia Zuhura eti sijui wangekuwa Ulaya wao Yanga saa hii ndio wangekuwa bingwa! Mwinyi na akili yeke huo ubingwa labda katika ndoto yake!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic