May 5, 2019


WINGA wa Kulia wa kikosi cha KMC, Hassan Kabunda amesema kuwa hana tatizo na uongozi wa Yanga endapo watafuata taratibu zote za usajili.
Kabunda ni miongoni mwa wachezaji machachari uwanjani kwani ukiachana na Ibrahim Ajibu menye pasi 17 ambaye ni kinara wa kutupia pasi za mwisho anayefuata ni Kabunda mwenye pasi 10.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kabunda amesema kuwa kazi yake kubwa ni mpira na hana mashaka na timu yoyote itakayohitaji saini yake yupo tayari kutua endapo itafuata taratibu.
"Mkataba wangu ndani ya KMC unakatika, nilisaini mkataba wa mwaka mmoja hivyo kwa sasa ndo namalizia, kama kuna timu inanihataji nipo tayari kuitumikia mimi ni mchezaji na ninajiamini.
"Yanga wakija sina tatizo mbali na kuwa ni timu kubwa kikubwa tunatazama malengo na mipango iliyopo na ni ndoto za wengi kufikia mafanikio, ninaamini wakifuata utaratibu na tukafikia makubaliano nitakwenda Yanga," amesema Kabunda. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic