May 3, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa leo dhidi ya Mbeya City utakaochezwa uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.

Simba jana walitia timu mkoani Mbeya na walifanya mazoezi ya mwisho jana kabla ya leo kuivaa Mbeya City.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema wapo tayari kuvaana na wapinzani wao Mbeya City kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya.

"Tupo sawa kuivaa Mbeya City, tunawaheshimu wapinzani wetu ila hakuna namna lazima tupambane kupata matokeo, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti na wasisahau kutoombea dua," amesema Manara.

Simba imepishana na kinara wa Ligi Kuu Bara kwa jumla ya pointi nane mpaka sasa, kwani Yanga amefikisha baada y kuchza michezo 34 ana pointi 80 huku Simba akiwa na pointi 72 baada yakucheza michezo 28.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic