KOCHA wa timu ya Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa amejipanga kuwatibulia mipango ya kubeba kombe la Shirikisho kwa kuwafunga Yanga Jumatatu.
Yanga itamenyana na Lipuli Mei 6, 2019 kwenye mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) uwanja wa Samora.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa wameweka kambi maalumu kwa ajili ya mchezo wao muhimu na wamejipanga kupata matokeo.
"Tumejipanga baada ya kupoteza mchezo wetu wa ligi mbele ya Biashara United, tunasahau yote sasa ni mwendo wa kuiwinda Yanga, kikubwa tunahitaji ushindi ili tutinge hatua ya fainali na tumeweka kambi maalumu," amesema.
Mshindi wa mchezo wa Jumatatu atamenyana na mshindi wa mchezo wa leo kati ya Azam FC na KMC utakaochezwa uwanja wa Chamazi.

0 COMMENTS:
Post a Comment