May 5, 2019


ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya unyekiti katika klabu ya Yanga Mbaraka Igangula amejitoa kugombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa leo Jumapili.

Igangula amesema amefanya uamuzi huo baada ya kugundua kuwa kuna uvunjifu wa katiba ya klabu ambapo wasimamizi wa uchaguzi kuruhusu watu wasio na sifa kugombea ama kushiriki kupiga kura.

Alieleza kuwa kuruhusu watu wasio na sifa kushiriki uchaguzi ni uvunjifu wa katiba na kwamba zipo kanuni za kikatiba zinazoeleza wazi mtu mwenye sifa za kushiriki uchaguzi.

Alienda mbali zaidi kwa kusema, kuna wanachama wanaenda kuchukua kadi ya Uanachama kupitia Benki ambazo zinaonyeha kumilikiwa na benki hizo kinyume cha katiba ambayo ndiyo roho ya klabu.

“Yapo mengi yaliyojili kwenye klabu yetu ya Yanga hususani ubadhirifu mkubwa wa pesa jambo ambalo linapigwa vita na Raisi wetu Dkt John Pombe Magufuli.

“Kwa hali hiyo ya uvunjifu wa katiba hiyo, kama nilivyoainisha, mimi Mbaraka Hussein Igangula, natangaza rasmi kujiengua katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo unaoendeshwa kinyume na katiba, hii ni katika kuilinda na kuiheshimu katiba yetu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic