May 30, 2019


Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba umepanga kuwatoa kwa mkopo nyota wake watatu akiwamo mshambuliaji, Adam Salamba, anayekwenda kukipiga nchini Ureno.

Taarifa imeeleza kuwa Salamba ambaye alisajiliwa na Simba msimu huu akitokea Lipuli FC kwa dau la Sh milioni 40.

Mchezaji huyo amekosa namba ya kudumu katika kikosi hicho cha Msimbazi kinachonolewa na kocha, Patrick Aussems, kutokana na kushindwa kumudu ushindani uliopo.

Adha taarifa imesema uwepo wa washambuliaji hatari kikosini hapo kama vile Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi, ulikuwa ni sababu tosha kwa Salamba kushindwa kutamba ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa wachezaji wengine ambao wanatarajiwa kutolewa kwa mkopo ni Rashid Mohammed, anayekwenda nchini Kenya na Abdul Mohammed, ambaye haijajulikana atakwenda timu gani.

Aidha, chanzo hicho kilieleza kwamba, tayari Aussems amekabidhi ripoti yake kwa uongozi inayoonyesha wachezaji watakaoachwa lakini hakuwataja kwa majina.

Hata hivyo, mtoa taarifa huyo alisema alichoeleza kocha ni kwamba wataachwa wachezaji wanne wa kigeni na watatu wazawa.

6 COMMENTS:

  1. Simba mnaharibu sasa hawa vijana ndio nguzo ya timu baadaye lakini mnawaondoa....hii haina afya kwa maendeleo ya timu angalau wangekaa misimu 2 ndio uwatoe kwa mkopo wengine hata misimu 2 hawajamaliza wanasepa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao madogo lazima watoke hapo ili wakape mechi nyingi zaidi.. wakibakia hapo Simba sc watakaa bench na vipaji vyao vitadumaa!

      Delete
  2. Hao wanapelekwa nje kuzidi kunolewa uwezo wao Kama vile wanapopelekwa watumizi WA uma kuongeza uwezo wao na uwezo WA Simba kuyatimiza hayo ni mkubwa na ndipo Simba inapozidi kunoga na wapo wanaojaribu kuyapindisha mambo kila wanapoona Simba inazidi kupata international admiration and recognition wao wanapata maumivu lakini wataanguka Chali kama mende

    ReplyDelete
  3. Kuwatoa kwa mkopo nje ya nchi ni jambo jema kwa kuwapa international experience hata wakirudi watakuwa wamepevuka kiakli na kujua nn wanakifanya,sio kila jambo kulaumu kila kitu.Lakini yote kwa yote tusubiri taarifa rasmi kutoka kwa uobgozi.

    ReplyDelete
  4. Pia hata hao wazawa wanaopelekwa kwa mkopo ni sahihi kabisa ukiachana na Salamba ambae kapewa muda mwingi wa kucheza bila mafanikio,Mohammed Rashid ameshindwa kuonekana huko alipo kwa mkopo KMC na dogo Abdul mohammed suleiman kashindwa kujitambua kama mwenzie Rashid Juma.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic