May 30, 2019


Klabu ya Yanga imeendelea kuonesha makucha yake baada ya kumalizana na kiungo Patrick Sibomana kutoka Rwanda.

Yanga imezidi kuboresha kikosi chake kutokana na wachezaji wengi kumaliza mikataba yao msimu huu uliomalizika.

Sibomana anakuwa mchezaji wa tatu kumwaga wino Yanga baada ya Papy Tshishimbi na Issa Bigrimana kumalizana na timu hiyo.

Usajili huu umekuwa pendekezo la Kocha Mwinyi Zahera ambaye amekabidhiwa majukumu ya kuhakikisha anapendekeza wachezaji wanaopaswa kusajiliwa.

7 COMMENTS:

  1. Leta visu,leta visu tukate mikia,Angalau tunaonyesha dhamila yetu, Hii ndio Yanga bwana! wenye kusoma wataisoma namba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwahiyo huu usajili mnaufanya kwasababu ya Simba sc? Kweli nyie vyura..

      Delete
  2. Usajili kitu kimojawapo ila perfomance ni kitu kingine. Mnaweza kutaka kukata mikia mkajikuta mnakata kandambili zenu. Msajili ili kuleta mapinduzi ya mchezo nchini, siyo kumkamia mtu fulani.

    ReplyDelete
  3. Yanga tupe raga wenye wivu wanywe sum, maana povu lilisha anza kuwatoka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Subirieni mwone mashine zitakazo shuka pale msimbazi ndio mtajua nini maana ya usajili wa kushiriki klabu bingwa upoje!

      Delete
  4. Simba kimyakimya bila ya kuropokwa na akiibuga kila mmoja ataufyata na kujiona si chochote si lolote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic