May 12, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa ili Tanzania kuwe na maendeleo ya soka inapaswa waamuzi wafuate sheria 17 za mpira pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania kutoa adhabu kwa wakati kwa wale wanaokiuka utaratibu.

Zahera amekiongoza kikosi cha Yanga kwa mafanikio makubwa ambapo mpaka sasa kipo nafasi ya pili kikiwa kimejikusanyia pointi 80 baada ya kucheza michezo 35.

Zahera amesema kuna mambo mengi ambayo yanatokea kwenye soka yanawaumiza wachezaji pamoja na viongozi wa timu hivyo ili kuleta maendeleo yapaswa kuyafanyia kazi.

"Kuna mambo mengi ambayo yanaendelea hapa kwenye ligi, nadhani kama waamuzi watakuwa wakichukuliwa hatua baada ya kukiuka sheria italeta msaada hapo baadaye kwani wengi watakuwa makini na kuifanya ligi kuwa na ushindani.

"Pia wahusika wenyewe wakijali na kufuatilia haya ambayo yanatokea kwenye ligi tutakuza mpira,ila kama hakuna anayejali basi tutabaki kurudi nyuma na kuishia kuwa wasindikizaji kwenye mashindano ya kimataifa," amesema Zahera.

2 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Huyu Kocha ndio maana anatakiwa asimamiwe na asiwafanye Yanga wote ni wajinga haiwezekani atamke kuwa eti atasajili wachezaji 8 tu....hata asiye na akili na soka anaelewa kuwa Yanga imekuwa dhaifu mno na zaidi ya 3/4 ya wachezaji waliopo kikosini hawafai hata kuendelea kubaki Yanga....sasa atakujaje na kusema atasajili wachezaji 8 tu? Ndio maana wanayanga wanahamasishwa kuchangia na kukusanya fedha ili waunde timu imara na kusajili wachezaji bora wa kutosha waondokane na hali iliyopo...tatizo halitakuwa pesa tena kwani watakuwa na fedha ya kutosha kusajili na kulipa mishahara....asiwafanye wanayanga warudi kule walipotoka kwa kuwa na kikosi dhaifu chenye wachezaji wa nje na ndani ya nchi ambao wengi wao ni magarasa wa kiwango cha chini ambao hata wakicheza na Lipuli, Ndanda, Singida United wanafikiria "kupaki basi". Yanga wanataka wachezaji wa kiwango cha juu mno wakushindana na kutoa upinzani wa hali ya buy kwa timu kama Simba, TP Mazembe, Al Ahly nk...hata kama hawata shiriki mashindano ya CAF lakini wataisaidia kuchukua ubingwa wa ligi hayo ndio matamanio na mahitaji yao wapenzi na wakereketwa wa Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic