May 21, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewashangaza vilivyo viongozi wa klabu hiyo baada ya kuwaambia kuwa alikataa mshahara wa dola 15,000 kwa mwezi (zaidi Sh 34 milioni) ili tu aendelee kuifundisha timu hiyo na kuhakikisha mipango yake aliyoianzisha inasimama.

Zahera ambaye alijunga na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita, alisema kuwa timu ya soka ya Buildcon ya nchini Zambia ndiyo Iliyomtangazia dau hilo baada ya kuvutiwa na uwezo wake.

Alisema Buildcon ilikuwa tayari kumpatia mshahara huo kwa mwezi lakini kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo dhidi ya Yanga pamoja mipango ambayo ameainzisha klabuni hapo, akaamua kuipotezea ofa hiyo.

“Jambo hili pia hata kocha Noel Mwandila (kocha msaidizi wa Yanga) analijua kwani baada ya Rais wa Buildcon kunipigia simu na kuniambia juu ya jambo hilo, nilimwambia.

“Lakini nilimwambia kuwa sipo tayari kuondoka Yanga kwa sasa na sababu kubwa ni hizo nilizojitaja hapo awali,” alisema Zahera.

3 COMMENTS:

  1. Duuuuuhh!!! Jamaa ni fix kweli kweli huyu

    ReplyDelete
  2. Uongozi mpya yaani umekuja na nuksi....wale Wanayanga wenye hasira wako wapi? Habari zinaendelea kuwa si nzuri sana wachezaji wote tegemeo wanaondoka wengine wakiuzwa na wengine mikataba ikiisha bila kuongezwa....jamani jamani hebu harakisheni kuokoa hali.....maumivu yanaendelea....hakuna habari njema wiki hizi mbili na mwezi mzima wa 5. Rekebisheni hali kwa kusajili at least mikataba ya awali ili kutoa moyo na kutia hamasa kwa wapenzi kuendelea kuchangia.....ukimya huu unaogopesha na ni hatari....mmeshaijenga chuki kwa wanayanga kuna wadau wa Yanga hawajitokezi kusaidia kwa kuwa tu hakuna dalili za kuanza kuleta mashine za uhakika hakuna hata mikataba ya awali kwa washambuliaji wakali na viungo wakali au mabeki wakali....Kuna kundi kubwa limeandaa fujo hawa ni wanachama ambao hawapendi hizi habari za huzuni zinazoendelea (Ajibu anaondoka burr, Makambo anauzwa, wachezaji 7 wanaumwa kuikosa Mbeya City, ubingwa kuchukuliwa na Simba, Sportspesa kuileta Sevila kucheza na Simba na siyo Yanga...nk. Na habari mbaya ndio zinazoendelea) Sasa amani ya nchi itavurugika....kwa kuwa kuna watu wanaumizwa na hizi habari...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic