May 21, 2019


KOCHA wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa aliuziwa mbinu na kocha wa Ruvu Shooting, Ablumutik Haji hali iliyofanya amshinde kwenye mchezo wa jana.

Said amesema kuwa kabla ya mchezo kocha wa Ruvu alitamba kwamba atatumia dakika 15 kujilinda kabla ya kuanza kushambulia hai iliyomfanya abadili mbinu.

"Kocha wa Ruvu alitamba kwamba atajilinda dakika kumi na tano za mwanzo sasa nikaamua kumpindua kwa kumlazimisha afunguke ndio maana nikapata matokeo kipindi cha kwanza.

"Ushindani kwa sasa ni mklai na kila timu inahaha kujiasua kushuka daraja hivyo ilikuwa ni lazima nishinde," amesema Said.

Biashara United ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 36 imejikusanyia pointi 43 huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 17 na ina pointi 42 baada ya kucheza michezo 37.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic