May 21, 2019


KIUNGO wa Simba ambaye ni kipenzi cha mashabiki, Jonas Mkude amesema kuwa kwa sasa hawana cha kupoteza zaidi ya kutetea ubingwa.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo imecheza michezo 35 na pointi 88 inahitaji pointi moja ili kutwaa ubingwa msimu huu imebakiwa na michezo mitatu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mkude amesema kuwa kwa sasa Simba hawana kitu kingine kitakachowarejesha kushiriki michuano ya kimataifa zaidi ya ubingwa hivyo wataingia uwanjani wakihitaji pointi tatu.

"Kwa sasa Simba hatuna kingine tulichobakiwa nacho mkononi zaidi ya ubingwa na hatuwezi kupata bila kushinda hivyo tutapambana kupata pointi tatu mbele ya Singida United.

"Tunajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na ushindani uliopo ila tumejipanga kupata ushindi, mashabiki watupe sapoti ili kuona namna gani tunashinda mchezo wetu," amesema Mkude. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic