June 10, 2019


BEKI kiraka wa kikosi cha Tanzania Prisons, Salum Kimenya amesema kuwa kwa sasa ni muda sahihi wa kupata changamoto mpya ili kujikomaza zaidi kwenye soka.

Kimenya amekuwa mhimili ndani ya kikosi hicho kutokana na kufanya majukumu yake kwa ukamilifu ambapo amekuwa ni kinara wa utupiaji ndani ya kikosi pamoja na kuwa namba moja kwa mabeki wenye mabao mengi msimu wa mwaka 2018/19 akiwa ametupia mabao 7.

Akizungumza na Salehe Jembe, Kimenya amesema kuwa maisha ndani ya Prisons yanampa faraja na anapenda namna wanavyoshirikiana ila kwa hatua ambayo amefikia kwa sasa ni wakati sahihi kupata changamoto mpya.

"Kupata nafasi ndani ya kikosi kikubwa kama Prisons sio kitu chepesi, naheshimu sana timu yangu na ninajua namna wachezaji wenzangu wanavyopambana kwa ajili ya timu ila kwa hapa nilipofikia naona ni wakati wangu kupata changamoto mpya.

"Malengo makubwa ni kucheza nje ya bongo kwa kuwa huko changamoto huwa tofauti na hapa, hivyo kama ikitokea mipango ikiwa sawa nitaweka wazi sehemu nitakayokwenda kucheza," amesema Kimenya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic