BEKI wa Yanga, Paul Godfery 'Boxer' kipenzi cha Mwinyi Zahera kwa sasa haelewi chochote kinachoendelea juu yake msimu ujao kutokana na kutopewa taarifa zozote ndani ya klabu hiyo.
Boxer msimu uliopita alionyesha uwezo mkubwa kwenye mechi zake alizocheza ambapo alikuwa mhimili kwa upande wa mabeki wa Yanga licha ya kupandishwa kutoka timu ya vijana.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Boxer alisema kuwa kwa sasa hajui hatma yake ndani ya Yanga na nini kinachoendelea juu yake.
"Ndugu yangu nashukuru Mungu nipo salama ila kwa upande wa mkataba wangu ndani ya Yanga sijui chochote kwa kweli, niponipo tu kwa sasa," alisema Boxer.
Wakuu bado sana anamktaba huyo mkumbusheni kwamba alisign miaka mitatu
ReplyDeleteAnajipendekeza simba na anatufaa kweli
DeleteMhh habari sijaiielewa mm najua bado anamkataba
ReplyDelete