June 8, 2019


UONGOZI wa KMC umesema kuwa mazungumzo yao na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije ambaye alijiunga na kikosi hicho msimu wa mwaka 2018/19 ambaye mkataba wake umemalizika mwezi Juni yamegonga mwamba hivyo wamemruhusu kuondoka.

Mwenyekiti wa Bodi ya KMC, Meya Mstahiki, Benjamin Sitta amesema kuwa baada ya kumaliza mkataba walimwita mezani Ndayiragije akagoma kuongeza mkataba mpya.

"Tunaheshimu mchango wake na tunajua kwamba kazi yake ni nzuri ila kwa sasa amesema hayupo tayari kuongeza mkataba mpya na ameomba kupata changamoto mpya hivyo tunamtakia kila la kheri huko anakokwenda.

"Kwa sasa tunajipanga kumleta kocha mpya ambaye atavaa viatu vyake hivyo tunaimani tutampata, hesabu zetu ni kwa yule mwenye uwezo wa kimataifa kwani kwa sasa tunajua tutashiriki michuano ya kimataifa," amesema Sitta.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic