June 21, 2019


Klabu ya Simba imepanga kuwatema wachezaji saba wa kigeni ndani ya klabu hiyo, imeelezwa.

Wachezaji wanaotajwa ni kiungo Haruna Niyonzima, James Kotea raia wa Ghana, Juuko Murshid na Emmanuel Okwi wa Uganda.

Ikumbukwe kuwa wachezaji hao wote mikataba na klabu ya Simba imeisha hivyo wako huru kwenda popote pale kuanzia sasa.

Taarifa imeeleza wengine ambao panga la Aussems linawapitia ni Nicholas Gyan raia wa Ghana, mabeki ni Asante Kwasi ambaye mkataba wake na klabu ya Simba utaisha December 2019 pamoja na Zana Coulibaly ambao mikataba yao inavunjwa ndani ya klabu hiyo.

Inasemekana wachezaji pekee wenye uhakika wa kubaki ni Mshambuliaji Meddie Kagere, Kiungo Clatous Chama na Beki Pascal Wawa.

8 COMMENTS:

  1. Kumwach kotei ni kosa kubwa sana....simba mlifikirie tena hili...kiungo bora wa club annachwa mbon haingii akilin

    ReplyDelete
  2. Haachwi mimi nawajuwa viongozi wa simba sc wako vizuri hawawezi kuwa na vichwa maji wakamuacha Kotei ili asajiliwe nani bora zaidi yake!

    ReplyDelete
  3. hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, habari za simba nyie mnazipata wapi acheni kutushika maskio usajili tu mpaka msubiri saa saba kama sisi.

    ReplyDelete
  4. Sasa watu mnalalamikaaaa.... Hivi kama huyo Kotei mwenyewe ndo kaona sasa basi kaomba aondoke mtamkatalia..??
    Acheni kuchambua soka kama mnavyochambua karanga na mchele!

    ReplyDelete
  5. Acha kutuongopea, juzi umesema Chirwa kaachwa Azam matokeo yake leo wanasaini mkataba. Tatizo unaandika vitu ili kuuza tu bila kujua kuwa unawachafua watu!!

    ReplyDelete
  6. Siku Haji au CEO akitangaza majina ya walioachwa hapo nitaelewa wengine mnachofanya ni habari za udaku.

    ReplyDelete
  7. Kwa kiungo kilichosajiliwa jana.. utamsahau kotei

    ReplyDelete
  8. Simba haimkstalii mchezaji kuondoka Hadi kufika Kwa wazazi wake. Akitaka kuondoka anafunguliwa milango yote miwili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic