June 21, 2019


Imebainika kuwa Simba walikuwa wanawaonea wivu Yanga baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Jumamosi iliyopita kutangaza kuipa Yanga uwanja maeneo ya Kigamboni jijini Dar.

Makonda alitoa ahadi hiyo katika hafla ya Kubwa Kuliko ambapo Yanga iliendesha harambee ya kuichangia klabu yao.

Wivu huo wa Simba umebainika jana Alhamisi baada ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kumuomba Makonda na wao awapatie uwanja kama alivyofanya kwa Yanga.

Manara aliyasema hayo jana wakati akitoa neno la shukrani kwenye hafla ya kuichangia Taifa Stars iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Dar.

Manara alisema kutokana na Simba kufanya vizuri msimu uliopita ikiwemo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika basi na wao wafikiriwe katika kupongezwa.

“Hata sisi tuna nyongo na wivu, wenzetu kule umewapa ekari saba, sisi tunakuomba hata tatu, hivi kweli timu imefika hadi robo fainali unatuacha hivihivi,” alisema Manara.

9 COMMENTS:

  1. Yanga ipo kisiasa zaidi. Wahusika wawe na tahadhari nakusudia viongozi wenye majukumu ya umma katika kuwatumikia wananchi sawa bila ya kuleta hisia za kibaguzi kwa upande mwengine lazima kuwepo na balanzi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Balance sio balanzi!! Ni usawa upi unaozungumzwa, mbona mnakuwa kama wanawake? wakati Kikwete analipa zaidi ya mill 35 kwa ajili ya simba kununua uwanja Bunju kulikuwa na balance?

      Delete
  2. Mzee JK alisema ukiwa Kiongozi hawa wote wako. Makonda anapaswa kuwapa pia Simba uwanja kama huo waliopewa Yanga ili kuwa fair

    ReplyDelete
  3. Mo alipochukua timu moja ya ahadi zake ni kuitafutia Simba eneo la uwanja,kabla hamjaomba Makonda awapatie eneo muulizeni kwanza Mo ahadi yake imeishia wapi vinginevyo Mzee Kilomoni ana hoja

    ReplyDelete
  4. Yaaani shida yetu ni kufikiria mabaya kwa mwingine,J.K asingesema mngejua wapi,R.C amewasaidia maana pale ni bwawa la samaki.
    Kwanza R.C amefanya jambo jema kwa dhana ya Uongozi.Manara alitoa hoja tu sasa kebehi zatoka wapi?
    Tujadili mambo kwa weledi tuache mihemko.

    ReplyDelete
  5. Afadhali Yanga wana eneo kubwa japokuwa wakati wa masika hugeuka kuwa bwawa la samaki lakini inawezekana kudhibiti maji pindi wakiamua lakini pale Msimbazi hata sehemu ya kujihifadhi hamna maana wakiingia ndani watu hamsini pamejaa na barabara inakatiza mlangoni matokeo yake mashabiki wanaishia kujazana kwenye vibaraza vya majirani na kuwa kero.......

    ReplyDelete
  6. Manara wewe umesema gongo wazi,umesema watembeza bakuli ,sasa mwenzako kapata wewe mbona mate mdomoni?

    ReplyDelete
  7. Miaka yote mmeshindwa kudhibiti mtaweza sasa,hizo ndoto,Haji atawapa taabu saaana.

    ReplyDelete
  8. siasa za siasa..twend kaz nothng under the sun has no source..usione ukadhan hii tz bhana..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic