MCHEZAJI AMBAYE HANA UHAKIKA WA KUONGEZEWA MKATABA AIPA YANGA STRAIKA WA SWEDEN
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe ameitaka klabu hiyo kumsajili straika wa Mwadui FC, Salum Aiyee kwani anaweza kusaidia lakini imevuja kwamba anakwenda Sweden.
Tambwe ambaye ameitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa ndani ya miaka mitano hana uhakika wa kubaki Yanga kwani mkataba wake umeisha na taarifa zinasema ni kati ya wachezaji wanaotemwa.
Aiyee anasifi ka kwa ubora wa kucheka na nyavu na msimu uliopita alitupia kambani mara 18 kwenye ligi kuu na kumaliza nafasi ya pili, kinara alikuwa Meddie Kagere wa Simba aliyofunga 23.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe ambaye sasa yupo nchini kwao Burundi, alisema kuwa Aiye ni mmoja kati washambuliaji wazuri wa ndani ambao anaamini wanaweza kufanya makubwa kama watalelewa vizuri kutokana na uwezo wake kucheza soka alionao.
Alisema, kama Yanga wanataka kusajili mshambuliaji mzawa mwenye uwezo wa juu basi wamsajili Aiyee mwenye umiri wa miaka 21 hivi sasa.
“Nipo nyumbani huku Burundi lakini mpaka sasa sijapata simu yoyote kutoka kwenye uongozi wa Yanga inayohusiana na mkataba mpya. “Hata hivyo, nichukue nafasi hii kuwashauri viongozi wa Yanga kama wana mpango wa kusajili mshambuliaji mzawa basi Aiyee ndiye anayefaa kutokana na uwezo wake, anajua kufunga pia ni mjanja sana anapokuwa katika eneo la hatari.
“Binafsi ndiye mshambuliaji mzawa aliyefanya vizuri kuliko wengine wote, lakini pia ameweza kuwa juu ya John Bocco pamoja na Emmanuel Okwi ambao niliamini kuwa wangemaliza wakiwa juu lakini amewatupa mbali japokuwa anatokea katika timu ya chini,” alisema Tambwe.
AIYEE SWEDEN Safari ya Salim Aiyee imeiva ambapo leo Jumamosi anakwenda nchini Sweden kwenye majaribio ya wiki mbili ya kucheza soka la kulipwa.
Aiyee ameliambia Championi Jumamosi kuwa, baada ya kumaliza taratibu zote za pasipoti ya kusafi ria leo Jumamosi atasafi ri kuelekea nchini Sweden kufanya majaribio ya wiki moja hadi mbili kwenye moja ya timu ambayo inashiriki ligi kuu nchini Sweden.
“Nishamaliza taratibu zote za kuhusu kusafi ri hivyo kesho (leo) Jumamosi nitaondoka kuelekea Sweden ambapo nitafanya majaribio ya wiki moja hadi mbili katika moja ya timu inashiriki ligi kuu nchini humo,” alisema Aiyee
0 COMMENTS:
Post a Comment