IMEELEZWA kuwa uogozi wa Ndanda FC umeingia kwenye harakati za kuinasa saini ya mshambuliaji wa Mwadui FC, Salum Aiyee kama ilivyo kwa Yanga, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho msimu ujao.
Aiyee amekuwa bora kwa msimu wa 2018/19 baada ya kuwakimbiza wazawa wote kwa utupiaji ambapo ametupia jumla ya mabao 18 ambayo ni mara yake ya kwanza kuyafikia tangu aanze kucheza soka la ushindani.
Akizungumza na Salehe Jembe, Aiyee amesema kuwa kwa sasa ametuliza kichwa ili apate timu ambayo itamfaa kwani ofa mkononi mwake ni nyingi.
"Mimi ni mchezaji na msimu uliopita nimepambana kwa ajili ya timu yangu na matokeo yake kwa sasa nina ofa nyingi, wakati ukifika nitasema ni timu ipi nitakwenda," amesema Aiyee.
Miongoni mwa timu ambazo amekuwa akihusishwa kwenda ni pamoja na Azam FC, Yanga, Alliance, Polisi Tanzania na Singida United.
0 COMMENTS:
Post a Comment