Kocha wa Algeria Djamel Belmadi amethibitisha kuwa amemtema kikosini kiungo mshambuliaji Haris Belkebla kwa utovu wa nidhamu. Kikosi cha Algeria kinaendelea kujifua kwaajili ya michuano ya Afcon, na kocha Belmadi amesema nidhamu ndio kipaumbele kwa sasa.
Mbadala wa Belkeba kwenye michuano hiyo itakayoanza Juni 21 ni mshambuliaji mzawa wa Ufaransa Andy Delort.
Kwa mujibu wa BBC. Tayari msahambuliaji huyo ameshatua kambini nchini Qatar.
“Kocha wa timu ya taifa Djamel Belmadi ameamua kumuengua kiungo Haris Belkebla kutoka kwenye kambi ya Afcon.
“Maamuzi ya kocha ni kwaajili ya kudumisha nidhamu miongoni mwa wachezaji, kitu ambacho kwake ni kipaumbele,” shirikisho la mpira la nchi hiyo limesema kwenye taarifa yake.
Hatua hiyo imefuatia picha ya video ya Belkebla inayomuonesha mchezaji huyo akionesha makalio yake kwenye mitandao wa kijamii.
Tukio hilo lilitokea wakati mchezaji mwenzake akiwa anacheza mbashara’gemu’ kwenye mtandao wa kijamii.
Kiungo huyo wa klabu ya Brest tayari amaeshaomba msamaha akisema tukio hilo limemuacha akiwa “amevunjika moyo”.
“Ningependa kuwaomba radhi. Hakika sikujua kwamba nilikuwa naoneka mbashara kwenye mtandao wa kijamii, hata hivyo, kile nilichokifanya kilikuwa nje ya maadili, na hakina nafasi kwenye mkusanyiko kama ule wa maana,” ameandika kupitia mitandao yake ya kijamii.
“Si nia yangu kujitetea kwa makossa niliyofanya, na tayari ninayalipia kwa kuondolewa kwenye timu ya taifa.
“Nimevunjika moyo lakini ni adhabu halali kutoka kwa vyombo vinavyosimamia mpira vya Algeria. Hakika sina kinyongo kwa mtu yeyote isipokuwa nafsi yangu kwa kuwaangusha na kuwaumiza.
“Kwa unyenyekeu nawaomba msiihusishe familia yangu kwa kile kilichitokea, ambayo imenikuza kwa maadili mema kuliko kile nilichokifanya.
“Maadili yangu ni makubwa na yapo karibu kabisa na madili ya taifa letu. Kwa mashabiki wote, wafanyakazi wa timu, wachezaji, familia yangu na kocha.
Belmadi, kikubwa ni kuwaomba radhi. Kwawachezaji wendangu, ndoto kwangu imeishia hapa, lakini natumai nitashangilia nanyi pale mtakaponyanyua kikombe. Idumu Algeria.”
Kwa mujibu wa BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment