December 15, 2018

 

TIMU ya  Simba imefungwa bao 2-1 dhidi ya Nkana FC kwenye Uwanja wa Nkana, Kitwe, Zambia unaobeba mashabiki 10,000 katika mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mabao ya Nkana FC yamefungwa na Ronald Kampamba dakika ya 27 kipindi cha kwanza na Kelvin Kampamba dakika ya 56 kipindi cha pili.


Simba wamepata bao  kupitia kwa John Bocco kwa mkwaju wa penati dakika ya 73 kipindi cha pili baada ya Meddie Kagere kuangushwa kwenye eneo la hatari.

17 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Kwa hali halisi ingawa nkana ana point tatu...lakini ni kama 2-2...bocco amefunga bao muhimu...Ingawa saleh jembe wamelibeza hilo

    ReplyDelete
  3. Kufuatana na Bin Zuberi..Simba anahitaji kushinda 1-0 ili afuzu..wamecheza hawakupaki basis!

    ReplyDelete
  4. Simba atapita mbona na wanaobeza watajuta kwa hilo.mungu ibariki simba mungu ibariki taifa stars mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  7. Mkuu Tino kujua kwamba Simba ikishinda 1-0 inapita hadi msikilize Bin Zubeir?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu unknown ingekuwa ni Yanga imepata hill bao la ugenini kichwa chaa hii habari kingepambwa na maneno kama wamefanya maajabu...tatizo LA Saleh jembe uandishi wao ni udaku tu na ulioelemea upande mmoja...watakuwa wamepata tabu sana Leo!

      Delete
    2. Sio bin zuberi...soma hata mwananchi...Saleh Jembe mnawabeza Simba waliokufa kishujaa lakini sana auheni mechi ya marudiano

      Delete
  8. Goal Moja La Bocc Ni Sawa Kupiga Ndege Wawili Kwa Jiwe Moja Asante Simba Kwa Kupata Goal La Ugenini Ni Imani Yangu Tuta Pita Taifa Kwani Hata Mazingira Ya Uwanja Wa Nkana Si Rafiki Kwa Soka La Safi La Simba Kwani Uwanja Ni Mdogo Na Wachezaji Wa Nkana Walitumia Rafu Na Nguvu Nyingi Uwanjani

    ReplyDelete
  9. Kama nyie ni mtandao unaopenda kutoa habari kwa watanzania....wekeni basis matokeo ya Mtibwa?Nyie mnajua tu Simba imefungwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. MTIBWA SUGAR WAONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA MICHUANO YA AFRIKA, WASHINDILIWA 3-0 NA KCCA LEO KAMPALA
      Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
      TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imechapwa mabao 3-0 na wenyeji KCCA katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Philip Omondi mjini Kampala jioni ya leo.
      Mabao ya KCCA, timu inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Kampala leo yamefungwa na Allan Kyambade dakika ya 48, Patrick Kaddu dakika ya 73 na Allan Okelo dakika ya 85.
      Mtibwa Sugar inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Zuberi Katwila ilizidiwa kabisa na KCCA kwenye mchezo wa leo.


      Wachezaji wa Mtibwa Sugar na KCCA katika mchezo wa leo mjini Kampala

      Kipigo hicho kinaiweka mguu nje Mtibwa Sugar kwenye michuano hiyo, sasa ikihitaji kushinda 4-0 kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo Uwanja wa Azam Complex mjini Dar es Salaam wiki ijayo ili kusonga mbele.

      Delete
  10. Mechi bado mbichi na mchezo wa mpira una matokeo matatu kushinda,kufungwa na matokeo ya sare ila Simba waiangalie sana beki yao bado kuna tatizo tena kubwa kulinganisha na umakini wanaotakiwa kuwa nao katika mashindano makubwa ya vilabu barani Africa kwani kila mechi ni fainali na ndivyo walivyoichukulia Nkana walivyojiandaa mechi yao na Simba.Mabeki wameruhusu mabo malaini au mepesi sana.Mabeki wameruhusu washambuliaji wa Nkana kupasua katikati ya moyo wa timu na kwenda kufunga yaani mchezaji anakokota mpira hatua kadhaa mbele ya mabeki one on one wanamsindikiza anakwenda kufunga. Kuna tatizo katika beki ya Simba kuanzia kiungo cha chini mpaka kwa senta half na sio kwamba si mabeki wazuri bali hakuna mawasiliano ya mazuri kati yao.Namuamini James kotei zaidi katika mechi za jihadi kuliko mabeki kadhaa wa Simba.Juuko ana matatizo yake lakini mechi kama hii ya Nkana si dhani kama Simba wangefungwa mabao mepesi kama yale.Mara nyingi punda mwenye mateke mkali ndie mwenye uwezo mkubwa wa kubeba mzigo sasa maamuzi yapo kwa mchungaji waache tu wamueke Juuko nje wakati anaweza kuwasaidia Simba isije yakawkuta ya Amunike na kichwa cha muenda wazimu cha taifa stars. Manula wanachokisema watu kuwa si mzuri wa mabao ya mbali na ya kushtukiza wanaelekea kuwa wapo sahihi. Ushindi wa Nkana wa mabao mawili kwa moja Simba wasichukulie poa hata kidogo kwani mechi yake ya kwanza kule msumbiji alishinda ugenini. Na inaonesha kabisa yakuwa Nkana wanabeki imara sana wanaweza wakaja kutafuta goli moja la ugenini kisha wakadifendi na uwezo huo wanao. Tunaimani wahusika watayafnyia kazi mapungufu yaliyoonekana kule kitwe.

    ReplyDelete
  11. ‘KAPTENI’ BOCCO AFUNGA BAO MUHIMU LA UGENINI KWA PENALTI SIMBA SC YACHAPWA 2-1 NA NKANA FC KITWE
    Na Mwandishi Wetu, KITWE
    SIMBA SC imepoteza mchezo wa kwanza wa hatu ya mwisho ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa 2-1 na wenyeji, Nkana FC Uwanja wa Nkana mjini Kitwe, Zambia.
    Sasa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watahitaji ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa marudiano Desemba 23 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo, ambayo mara ya kwanza na ya mwisho walifika mwaka 2003.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Salisu Basheer aliyesaidiwa na washika vibendera Peter Eigege Ogwu na Efosa Celestine Igudia wote wa Nigeria, hadi mapumziko Nkana FC walikuwa mbele kwa bao 1-0.


    Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Ronald Kampamba kwa shuti kali dakika ya 27 akimalizia pasi ya beki Muivory Coast, Ben Bahn Adama.
    Na kipindi cha pili Nkana FC walikianza vizuri na kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba SC hadi kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 56 kupitia kwa Kelvin Kampamba.
    Kocha Mbelgiji wa Simba SC, Patrick J Aussems alifanya mabadiliko baada ya bao hilo akimtoa mshambuliaji Emmanuel Okwi na kumuingiza kiungo Shiza Kichuya.
    Mabadiliko hayo yaliisaidia Simba SC kupata bao la ugenini, lililofungwa na Nahodha John Raphael Bocco kwa penalti dakika ya 74 baada ya mshambuliaji Myarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere kuangushwa kwenye boksi.
    Kikosi cha Nkana FC kilikuwa; Allan Chibwe, Hassan Kessy, Ben Banh, Musa Mayeko, Harrison Chisala, Ronald Kampamba/Festus Mbewe dk84, Walter Bwalya, Kelvin Kampamba, Richard Ocran, Duncan Otieno na Shadrack Malambo/Freddy Tshimenga dk86.
    Simba SC; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, James Kotei, Clatous Chama, Emmanuel Okwi/Shiza Kichuya dk60, John Bocco/Hassan Dilunga dk90+2 na Meddie Kagere.

    ReplyDelete
  12. Watanzania tunapenda sana kulalamika. Simba ilizidiwa kwenye baadhi ya idara...hasa pale Kati. Middle zilishndwa kuhimili vishindo vya middle wa Nkana. Na tujue bila kutoa heshima au kuwaheshimu wale jamaa na tukajiamini kiukwel tutakuwa kwenye nafasi ya kutolewa. Ni lazima tuoneshe heshima zetu kwao ili tutafutr njia sahih ya kucheza nao. Tusiamini kwamba kwa kuwa tumepata lile goli ndio tutaweza kuwatoa bila kutafuta mbinu bora ya uchezaji. Timu naiona ina mfumo mmoja tu haiwez kujityuni ndani yenyewe. Wachezaji ni lazma waoneshe ukomavu wa kutafuta mbinu mbadala endapo mbinu ya kwanza itakuwa imefel

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic