June 16, 2019


BODI ya Wakurugenzi ya Simba SC, Company Limited imetangaza rasmi kuanza usajili wa wachezaji wake wapya wakitumia ripoti ya kocha mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems.

Hiyo, ikiwa ni siku chache mara baada ya kumalizika kwa kikao cha bodi hiyo kilichofanyika juzi jioni kwenye moja ya hoteli kubwa kwa lengo la kuweka mikakati kadhaa na mambo hayo. Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Cresecentius Magori amefunguka ishu nzima:

USAJILI WA MSIMU UJAO

“Bodi imepokea na kupitisha maendeleo ya hatua ya usajili ilipofikia na imebariki kamati ndogo ya usajili iliyoteuliwa na mwenyekiti wa bodi.

“Usajili kwa wachezaji wa ndani umekamilika kwa asilimia 90. Taarifa za wachezaji waliosajiliwa zitakuwa zinatolewa kila siku kupitia ukurasa wetu wa klabu.

“Kama tulivyoanza kwa Bocco (John), Nyoni (Erasto), Manula (Aishi) na Mkude (Jonas) tuliyemtangaza leo (jana), hivyo
kesho (leo) tutamtambulisha mwingine mzawa.

MUUNDO WA KLABU

“Klabu ilijipa muda wa mpito wa kukamilisha ubadilishaji wa muundo wa mabadiliko ya klabu kuwa kampuni. Bodi imeridhika na hatua iliyofikiwa ya ukamilishaji wa muundo.

“Bodi imewateua Aziz Kefile, Mulamu Ng’ambi, Barabara Gonzalez na wanasheria wa kampuni wa Simba, Evodius Mtawala na Michael Mhina kukamilisha kwa haraka hatua ndogo iliyobakia na ndani ya miezi miwili itakuwa imekamika.

BUNJU PROJEKTI

“Bodi imepokea taarifa za maendeleo ya sehemu ya mazoezi ya timu iliyokuwepo Bunju na baada ya mvua matengenezo ya uwanja huo haraka yanaanza kwa kuweka nyasi bandia na ujenzi wa vyumba vya kubadilishia nguo na uwanja wa nyasi za kawaida.

MAANDALIZI PRESEASSON

“Wakati wowote taarifa za timu wapi itakwenda kuweka wapi itawekwa wazi kwa kwenda nje ya nchi na bodi tayari imeunda tume ya kamati ndogo kufanya maamuzi.

“Tumeandaa Simba Wiki itakayoendana na Simba Day ambayo hufanyika kila mwaka, tumepanga kucheza na klabu moja kubwa kutoka Afrika Magharibi.

3 COMMENTS:

  1. Nina hofu Sana Na usajili WA simba maana imefanikiwa Tu kubaki Na hadhi ya kondoo wake muhimu mchezaji mpya mpaka sasa kutoka ndani Ni kakolanya hao wengine bado hawajamalizana kasema yanga wako makini kuliko simba huu ukimwa haina lolote mbona kwa kakolanya wameweka wazi.

    ReplyDelete
  2. Tunasajili kimataifa sio kama chura

    ReplyDelete
  3. Sioni sababu ya Simba kukimbilia kusajili.Ninachoamini Simba inazingatia ripoti ya kocha wao na pia Yanga inasajili kufuatana na maelekezo ya kocha wao.Huwezi kumlazimisha kocha wa timu fulani afuate yale yanayofanywa na kocha wa timu nyingine.huo utakuwa ni uwendazimu.Simba ya sasa ninavyoiona haina haja ya kusajili lundo la wachezaji wapya zaidi ya watano.Na kama Simba inataka kujiamarisha basi kwa maoni yangu ni mabeki wa kati na wenye nguvu
    beki,kiungo mkabaji na washambuliaji wawili










    na Yanga anasajili kufuatana na maelekezo ya kocha wao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic