June 21, 2019





Mabingwa wa soka Tanzania, Simba wameongeza nguvu katika safu yao ya ushambulizi baada ya kumsajili, Wilker Henrique da Silva kutoka nchini Brazil.


Wilker amejiunga na mabingwa hao akitokea nchini Brazil.



Uongozi wa Simba umesema umesaini mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji huyo.


Maana yake Mbrazil huyo anaungana na John Bocco, Meddy Kagere na wengine kuimarisha safu ya ushambulizi ya mabingwa hao.


Simba imepania kufanya vizuri Afrika na kuiska mbali zaidi katika ligi ya mabingwa.


Msimu uliopita, Simba ilifika katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuifanya Tanzania kuongeza timu mbili za michuano ya Caf, upande wa klabu.

10 COMMENTS:

  1. Ebwanae kitu na box hicho upande wa pili mpooooooooo...?

    ReplyDelete
  2. Simba wanafanya bila ya kumfanya kelele Ila unashitukia tu MTU goli na mambo ndivo jinsi yatokuwa

    ReplyDelete
  3. Hapo vipi hapo sawa nimemwangalia you tube yuko vizuri

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli jamani Simba hii sasa fujo kha. Sisi Yanga tulikuwa tukiwatania tu hatukutaka mfike huko mtakuja kutuumiza mjuwe��

    ReplyDelete
  5. Timu inavurugika. Mnawaondoa juuko, okwi, Agei, gyan na kwasi mnaleta watu ambao hamjui performance yao itakuwaje ndani ya timu. Wachezaji wanaoondoka wote walikuwa kikosi cha kwanza (first eleven) na waliipeleka timu robo fainali club bingwa. Kwa taarifa yanga wanamchukua okwi na juuko, mtajuta.

    ReplyDelete
  6. Wacha uongo chura.Endelea na michango.

    ReplyDelete
  7. https://us.soccerway.com/teams/brazil/clube-atletico-bragantino/2827/ muangaliae umu katika kikosi kma yumo na hiyo ndio timu wanaosema ametokea

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sioni jina la mchezaji huyu Wilker Henrique kwenye mtandao huo.Ina maana you tube video anazoonekana huyo mchezaji ni za kutengenezwa na Simba imeshapigwa changa la macho na mawakala wapiga dili.Hivi kweli Simba hawana mascout wao wa kufuatilia wachezaji na inabaki kutegemea mawakala ambao wao wanachoangalia ni kufanya biashara asubuhi na mahesabu jioni.Isije tukajikuta tumebeba tena wale wachezaji aina ya kina Jaja.Anyway tusubirie vitendo uwanjani.

      Delete
  8. Licha ya malengo ya klabu bingwa Africa Simba huu ni wakati wa kufanya bishara kubwa ya wachezaji vile vile. Kwa usajili huu na kama mambo yatakwenda vizuri Simba itajijengea jina zaidi. Simba kama wagelitaka kuvuta pesa ndefu kwa kagere na chama wangeuza sana. Na ndio maana nasema wakati akina kagere na chama wanasajiliwa msimu uliopita kuna watu walipiga kelele na kubeza kuhusiana na gharama za manunuzi pamoja na matunzo ya wachezaji hao ila licha ya wachezaji hao kuchangia kwa kiasi kikubwa kuipandisha thamani Simba lakini thamani pia binafsi za wachezaji hao zimepanda mno na Simba kama ingelitaka kuwanunua kutoka klabu nyengine hivi sasa sidhani kama Simba wangelimudu kuwanunua. Na Kwa uzoefu huo wa akina kagere naona Simba watakuwa wamejifunza mengi na wakiwa smart Zaidi basi mwakani watakuwa na akina kagere kadhaa watakaotakiwa hadi na vilabu vya ulaya.Simba hata yule Bwalya Kama Nkana wangeshuka kidogo wangemnunua tu na hakika mwakani wangemuuza mara dufu ya bei walionunulia. Simba ni klabu maarufu sana hivi sasa na Kama vile haitoshi kocha wao alishawahi kuwapa wachezaji kadhaa chipukizi wa Simba nafasi ya kuwauza ubeligiji lakini masikini vijana wetu bure kabisa. Ausems kwa kauli yake kasema ana marafiki kadhaa makocha na wakurugenzi wa ufundi ubeligiji waliokuwa wakimuomba awatafutie akina Samata wengine Tanzania. Kwa hivyo katika usajili wao Simba wafikirie wachezaji kwa ajili biashara vile vile kwani Kwa Simba ya sasa kula ukitizama future yao kwa kweli ni ya kwenda juu zaidi na Mungu awabariki zaidi Amin.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic