June 23, 2019


Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kimepoteza mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kufungwa mabao 2-0 na Senegal.

Stars imepoteza mchezo wake ikiwa ni mara ya kwanza inashiriki mashindano hayo baada ya miaka 39 kupita.

Mabao ya Senegal yamewekwa kimiani na Keita Balde mnamo dakika ya 28 na Krepin Diatta katika dakika ya 64.

Ushindi huo wa Senegal unaiweka Taifa Stars katika nafasi ya nne ya msimamo wa kundi C huku Senegal ikishika nafasi ya kwanza ikiwa na alama tatu.

Wakati huo Kenya na Algeria wanakipiga baadaye majira ya saa tano kamili za usiku.


9 COMMENTS:

  1. TUSEME NINI SASA KAMA SIO KOCHA?

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha sana na sijui Amunike anachokifundisha kitu gani ndani ya Taifa stars. Hakuna ubishi Senegal ni timu kubwa kimpira zidi ya Taifa stars ila hata Misri ni timu kubwa zidi ya Zimbabwe isipokuwa tofauti wazimbabwe licha ya kufungwa na Misri wamecheza mpira mzuri kabisa. Mpira walioucheza Taifa stars zidi ya senegali ni mpira wa hovyo kabisa hakuna haja ya kumumunya maneno. Ila watu wakisema wahusika na wale wa kufuata mkumbo huja juu kwa ukali kumteta kocha na benchi lake ufundi.
    Anamueka nje Nyoni zidi ya Mwantika. Mungu bariki Refa alikuwa ni wa ajabu sana kwa kutochukua hatua stahiki zidi ya faulu za kipumbavu za taifa stars.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nilikuwa najichekea kwa soka la hovyoo waliokuwa wanacheza timu yetu ya Tanzania.Badala ya kusikitika unalazimika ucheke tu kwani hakuna jinsi na hakuna cha kufichwa maana yalionekana hadharani.Kuna wakati ukimwona Ramadhani Kessy au Mwantika unatamani umeme uwanjani ukatike.Ulimwengu ameflop na hana impact tena.Simzungumzii Fei na hana kosa lolote kwa sababu kiuhasilia kwangu Fei hajakomaa kuchezwa game kama hizi.Ni mchezaji wa kuingizwa dimbani zikiwa zimesalia dk 10 hivi hivyo makosa ni ya kocha Amunike.Ukiangalia ubao wa statics unaoanyesha Senegal possesion 82% na Aishi Manula 18% na huo ndio ukweli wenyewe.
      Siasa za bongo zinaingilia sana mchezo wa soka Tanzania na hii yote wanasiasa wetu wamekuwa na kiherehere ya kutaka kiki.Mwanasiasa mmoja alisikika kuwa atavalia njuga wachezaji wa kigeni wasicheze zaidi ya watano kwenye ligi na jana tumeona wachezaji walivyokuwa wanatafuta mpira kwa tochi licha ya Tanzania kuwa na wachezaji 12 uwanjani maana refa alitubeba sana na abarikiwe kwa kweli.

      Delete
  3. Unamueka nje mtu kama Nyoni na Mohamedi Hussein una kwenye inayohitaji wachezaji wazoefu unatarajia nini? Wacha tu Kocha ajifiche kwenye kichaka cha kutengeneza nidhamu.

    ReplyDelete
  4. Makosa ni pale tunapofananisha na kulinganisha kichuguu na mlima. Vijana wamejitahidi alau kupunguza idadi ya magoli ingelikuwa ile timu pendwa tungepigwa hata 6.
    Afadhali Haji Manara alisema kweli isiyopendwa na kina sisi

    ReplyDelete
  5. Mechi za mwanzo zimetupa picha halisi ya soka letu Africa Mashariki (Kenya, Tanzania, Burundi, Madagascar, Uganda & DRC)....."pumba na mchele vimejipambanua"

    ReplyDelete
  6. Hata Burundi wapo bomba kuliko taifa stars ya Amunike. Kabla ya mechi eti oh tutaifunga Senegal sasa hivi oh senegali ni timu kubwa,hovyo kabisa.Wachezaji wamejitahidi kwa jinsi wanavyojua wao hapana shaka ila kocha sie. Nchi hii kuna mabichwa mambumbu kweli kweli yaani pumba kabisa.Amunike alishatufelisha zamani sana na hakustahili kuachiwa timu kujiandaa na Afcon kwa sababu hakuwa na dalili yoyote ile yakwamba anaweza kuibadilisha Taifa stars ni kocha wa daraja la chini mno. Hao TFF ni wa daraja la hovyo miongoni mwa vyama vya mpira barani Africa kwa hivyo haishangazi kuona wanashindwa hata kufanya uteuzi wa kocha anaefaa kwa ajili ya Taifa. Wanaosema Tanzania ni ndogo zidi ya senegali kimpira subiri mpaka tutakapokuja kupigwa na Kenya ndio labda mtaamini kuwa hatuna kocha.

    ReplyDelete
  7. Tukumbuke kocha hajawai tangu azaliwe kufundisha timu ya taifa ykyote nje ya wale watoto wa Naijeria ambako wakamtimua. Kocha hana izoefu wowote kwa hiyo tumpe muda ajifunzie kwetu kupata uzoefu. Na yeye ni binadamu anahitaji uzoefu kupitia timu ya wabongo. Ebu fikiria Mwantika hajawai kucheza mechi za kimashindano na ni mtu wa benchi huko Azam lakini kwa stars hii ni LULU......nashindwa kuamini

    ReplyDelete
  8. Ni heri hata wangemchukua Piere Lechante baada ya mkataba wake na Simba kumalizika.Kocha alishafeli tangu Eswatin hata Mkuu alilihoji hill.
    Daaa masikini nchi yangu niipendayo Tanzania.
    Na hoja ya kusema Senegal wako mbali haina mashiko na ndiyo maana ya kwenda kushindana maana unajiandaa hujui utapangiwa nani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic