June 25, 2019


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa auhofii usajili unaoendelea kufanywa na watani wao wa jadi, Simba ukiwemo wa straika Mbrazili, Wilker Henrique da Silva.

Wiki iliyopita Simba ilimtangaza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo.

Yanga upande wake imefanikisha usajili wa wachezaji kumi kati ya hao sita ni wa kimataifa na watatu wazawa ambao ni Abdulaziz Makame, Mapinduzi Balama na Ally Ally. Kutoka nje ya nchini ni Issa Bigirimana ‘Walcott’, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Lamine Moro na Suleyman Mustapha.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliwataka watani wao Simba kuendelea kusajili Wabrazili akiamini ni wa kiwango cha kawaida kama walivyokuwa Wabrazili waliocheza Yanga, Andrey Coutihno, Genilson Santana Santos ‘Jaja’ na Emerson De Oliveira Neves Rouqe.

Mwakalebela alisema wao usajili wao wanaoendelea kuufanya utaendana na ligi ambayo inachezwa kwenye viwanja vibovu kabla ya kwenda kushiriki michuano ya kimataifa, mwaka huu kwa kusajili wachezaji wa ndani na nje ya nchi wenye uwezo na uzoefu ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.

Aliongeza kuwa wamepanga kufanya usajili mmoja mkubwa wa kishindo utakaofunga usajili wao kabla ya kuingia kambini kujiandaa na msimu mpya ambao wamepanga kurejesha heshima yao iliyopotea.

“Hakuna Mbrazili atakayekuja hapa nchini mwenye uwezo mkubwa wa kucheza ligi na kufikia hatua ya sisi Yanga kumuogopa, hivyo wakae wakifahamu hatuwaogopi tusubirie ligi ianze.

“Mbrazil anayekuja hapa ni wa kiwango cha kawaida, Wabrazili wa juu ni wale wanaokwenda kucheza ligi ya ushindani Ulaya na siyo hapa nchini ambayo miundombinu yenyewe ya viwanja ni vibovu.

“Hivyo, basi kama Wanayanga wasiogopeshwe na usajili huo unaofanywa na watani wao Simba, kikubwa wasubirie burudani katika msimu ujao kutokana na usajili mkubwa unaoendelea kufanywa na viongozi wao,” alisema Mwakalebela.

13 COMMENTS:

  1. Tutarudia mtindo wa kila mtu ashinde gem zake

    ReplyDelete
  2. YANGA lazima waogope kishindo hiki cha Simba.Na hii kauli ya Mwakalibela na dalili tosha kuwa Yanga wana hofu na usajili wa Simba wanatakiwa kutulia tu. Simba sio wapumbavu kwenda kujizolea wachezaji wa hovyo. Simba ya leo sio Yanga ile iliyokuwa ikijiokotea wabrazili wa hovyo lazima mtofaitishe kati ya kampuni na kundi la wajanja fulani waliokuwa wakipiga madili ndani ya Yanga ya Manji.

    ReplyDelete
  3. Yanga wameaswa WASIOGOPE!!! HIVI KUMBE WANAOGOPA? KAMA NI HIVYO UMEANZA WEWE MWAKALEBELA KUOGOPA!! TUKUTANE UWANJANI.

    ReplyDelete
  4. Hicho alichoongea mwakalibela kina dhihirisha kuwa yeye no mtu wa mpira sio kauli za kina manara au hata jerimuro aliekuwa msemaji wa yanga. Mm ktk vitu ambavyo siendekezi ni his kauli za kishabiki za kina manara au jerimuro kipind kile. Hao sio watu wa mpira niwavamiz tu wakunakshi ajira zao za isemaji.narudia Tena asimi ia kubwa ya wachezaji ambao asilimia 98 au 100 wanaweza kuonesha uwezo unaotarajiwa utawapata ndani ya afrika mashariki. Nje yapo tunabahatisha tu, sisemi kama hawapo lah, wapo wazuri wanaweza kupatikana nje ya afrika mashariki ila niwakubahatisha. Hakuna mchezaji mzuri kutoka afika magharib au kaskazini atakuja Tanzania, hakuna mchezaji mzuri wa uingreza, Brazil,hispein,itally au ufaransa atakaekuja Tanzania kucheza. Hata Hawa kina kibre cheche, kotei,kwasi,tumiwabahatisha tu labda kwakuto jitambua kwao. Tukumbuke hao kina kotinyo au Jaja, wote hawakuwa special Sana but hata Tanzania walikuewepo Zaid yao. Hatuwez kuwalaumu yanga kipindi kile Kwan lile lilikuwa agizo la kocha maximo. Sasa tujiulize kweli Simba wamekosa wachezaji makini ndani ya Kenya Uganda,Rwanda mpaka walete mbrazili? HIV kweli mbrazili anaejitambua na mwenye kiwango kizur chakucheza mpira ataacha kwenda hispin au England au hata Africa ya kusini tu nakuja Tanzania. Tafakiri acha ushabiki, tupambane kujenga ligi yetu kwa kusajili wachezaji bora tusije leta wauza matimiti maji hapa kwetu. (MWINA KADUGUDA) KATIBU MKUU WA ZAMANI WA SIMBA SC.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jitahidi kuandika kiswahili fasaha tukuelewe ndugu,pia majina ya watu unayaharibu

      Delete
    2. Maelezo yako tu automatically yanaonyesha udhaifu wako katika kuelewa mpira, alichoonyesha mwakalebela ni fear iliyopo moyon mwaka na mashabiki wake kwa kutambua ubora wa mchezaji husika na upinzani watakaokutana nao katika ligi, mpira ni mapambano tu jitihada na kujituma kwako ndio kutakufanya utoboe bila kujalisha unachezea timu gani, cha mno ni timu iwe inashiriki champion league tu kwani iyo inatazamwa na wengi xo ukikaza tu umetoka kimpira .

      Delete
    3. Wacha muda ufike tuone nani aliyesajili.. haya maneno mengine ni mbwembwe tu😆

      Delete
  5. Kama Simba wamesajili wachezaji wa kiwango cha chini, nyinyi Yanga inawahusu nini? Si mkutane uwanjani kujua yupi bora na yupi mbovu? Makamu mwenyekiti wa Yanga kuzungumzia usajili wa Simba, inakuhusu nini, zungumzeni yenu jamani!!!

    ReplyDelete
  6. haya simba wanakiwango cha chini...kila timu ifanye usajili wake na baadaye zicheze mechi zake....Mbona gongowazi wanaanza mchecheto!

    ReplyDelete
  7. Hivi vyura hata masika bado wameshaanza kukoroma.Sijawahi kusikia kiongozi wa Simba akitoa comments za usajili wa vyura.Viongozi wa Simba wanafuata ripoti ya benchi la ufundi na kocha wao Patrick Aussems na kocha amekiri kuwa wanawasiliana na wanajadiliana kuhusu wachezaji wanaosajiliwa.Kama Wabrazil wanaendelea kusinya na mmeshawahukumu ni wabovu then kwa nini mnalialia kabla hata ligi haijaanza?
    Mara wabrazil hawataviweza viwanja vyetu ni vibovu kwani hawo wabrazil watacheza mechi zote 38 za ligi?...Si kuna wazawa kina Kennedy watacheza viwanja vya Musoma,Singida.
    Na kwa taarifa uelewe nchini Angola kuna wachezaji wengi kutoka Brazil wanaocheza ligi ya Angola na hata Rivaldo alitoka klabu kubwa Barcelona na akacheza ligi ya Angola.Kila timu itavuna ilichopanda.

    ReplyDelete
  8. Na bado....tutakuja kusikia Simba anabebwa na TFF kwenye usajili maana inakuwaje Simba ana viporo vya usajili? Yanga ameshasajili wachezaji wapya 11 na Simba wachezaji 5 na Azam wachezaji 3....Tunasubiri mwezi wa August tuchane mikeka

    ReplyDelete
  9. Sasa vyura kelele za nn?😂 kwani simba tumemsemesha mtu?.. tulieni acheni kuweweseka.. Simba sii ya ligi hii..tunaenda kubeba CAF CL.Yanga huu usajili hauwahusu

    ReplyDelete
  10. Hawa jamaa ni woga na wana kitu kinaitwa hasada. Tamko kuhusu Simba linawahusu nini mbona Simba hawawaingilii, hawawaingilii kwasababu haijawahusu kitu. Badala ya kujishughulishia bakuli Lao wamekuwa wiparamia Simba kwakuwatakia mabaya. Mafanikio ya Simba yanawaumiza kiasi cha kuwarusha akili na kuropokwa ovyo. Kutokana na hasadi zao hawa jamaa wataanguka Vibaya katika ligi ijayo na kumbe la mabingwa Africa anbapo Simba ndio iliyowawezesha kushiriki na wataanguka kwasababu wanjishughulisha kuiutakia mabaya Simba na wanajisahau kujitakia mema wenyewe.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic