July 14, 2019

MABINGWA watezi wa kombe la Kagame Azam FC baada ya kutinga hatua ya robo fainali wameanza kujiwinda kuelekea kwenye mchezo wa robo fainali utakaochezwa Julai 16 dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Maganga amesema kuwa hatua ya robo fainali ni ngumu kwani timu itakayofungwa inatolewa jumla kwenye michuano.

"Kazi yetu kubwa ni kutetea ubingwa na hatua ambayo tupo kwa sasa ya robo fainali ni mtoano timu ikifungwa inafungasha virago.

"Timu ambayo tutacheza nayo si ya kubeza hivyo tumejipanga kupambana na kutafuta matokeo chanya Julai 16," amesema. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic