July 14, 2019


Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga yupo mbioni kumrejeshea kitambaa cha unahodha beki Kelvin Yonddani.

Hatua hii imekuja mara baada ya aliyekabidhiwa kitambaa hicho, Ibrahim Ajibu kutimkia Simba ambako amesaini mkataba wa miaka miwili.

Taarifa zinasema Zahera ameamua kufikiria kumrejeshea tena Yondan baada ya kumpoka siku za hivi karibuni kutokana na makosa ya kinidhamu.

Yondani ambaye pia aliwahi kuichezea Simba sasa kuna dalili kubwa za kuendelea kuvaa kitambaa hicho.

Beki huyo mkongwe wa Yanga na Taifa Stars atakuwa anashikilia kitambaa hicho kwa muda mrefu tangu akichukue kutoka kwa kaka yake Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye amestaafu soka.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic