July 29, 2019

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ushindani kwa ajili ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa tayari wameanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao.

"Tayari kikosi kimeanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao na tunajua kwamba ushindani ni mkubwa, hivyo nasi tunajipanga" amesema .

Azam FC itaanza msimu ikiwa na kocha mpya ambaye ni Ettiene Ndayiragije aliyekuwa KMC msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic