July 29, 2019

HAJI Manara ni kama amewatupia dongo wapinzani wake Yanga kiaina kutokana na kauli yake kwamba wengi wamewaiga siku ya Simba day na wameiga kwa mpango mdogo.

Manara amesema kuwa wengi wanaiga mpango wao wa kuwa na siku maalumu ya kuwatambulisa wachezaji na bado hawajafikia hatua ya ubora ambao Simba wapo kwa sasa.

"Wengi tunaona wanaiga, kuna wale ambao wapo Kenya, Uganda na sehemu nyingine tunaskia wana maandamano kabisa hivyo hayo ni maono madogo.

"Sisi tunakuja kikazi na kauli mbiu yetu ya Simba day msimu huu ni SpotiPesa Simba wiki, iga ufe, huwezi kuiga tu kitu bila ya kuwa na mpango mzuri, masuala ya maandamanomaandamano kwetu tulishamaliza kitambo tunaangalia mambo mengine, hii mambo sijui ya kusema namna gani vipi kwetu hakuna.

"Sisi ni hatua nyingine kabisa kwa sasa kuna watu wa Kenya, Uganda nao wanaiga hivyo tunafanya kazi kubwa, tumejipanga kisawasawa," amesema.



7 COMMENTS:

  1. Sawa Mzee,sasa kaa kimya sio unapofungua mdomo kitu unacho sema ni mambo ya yanga

    ReplyDelete
  2. Jiwe la gizani mara paap kuna chura anateseka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nani anatupa jiwe gizani?si wachawi,endelea kutupia jiwe

      Delete
  3. Umbea Mbea Tu Kama Vp Kausha Mzungu Wetu Mwenye Madongo

    ReplyDelete
  4. kwan kuna makosa kupta hosptalin kuwatakia watu hali na kutoa michango? kama mtu hayakuhusu funga domo lako na ile inaitwa cku ya wananch si yanga day ile na utaishia hvohvo.

    ReplyDelete
  5. Ni msemo tu."Kutupa jiwe gizani"Umetoka pori gani .Huu ni msemo makhususi kwa watu wanaojishuku.Simba ni level nyingine sasa. Saizi yako KMC na Biashara.

    ReplyDelete
  6. Ila cjaona sehem aliyotaj jina la team kasem kenya, uganda wanaig hivyo lazim wawe creative

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic