July 20, 2019


ATHUMAN Bilal ndiye mrithi wa mikoba ya Malale Hamsin aliyekuwa anakinoa kikosi cha Alliance FC.

Mwenyekti wa Kamati ya mashindano ya Alliance, Yusuph Budod amesema kuwa wamekubaliana kamati na kukubali uwezo wa Bilal hali iliyofanya wampe kandarasi ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao na atasaidiana na wengine ambao ni Kessy Mziray na Gilbert Dady.

"Tunaamini uwezo wa Bilal hasa ukizingatia alifanya vizuri alipokuwa na timu ya Stand United, imani yetu ni kuona anafanya maajabu msimu ujao," amesema.

Bilal alikuwa kocha wa Stand United ambayo imeshuka daraja na msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic