July 20, 2019


FRANK Kamugisha, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano ndani ya Yanga amesema kuwa mpango wa kuweka kambi nje ya nchi haujayeyuka kinachosubiriwa ni droo ya Caf kuchezeshwa kisha watakwea pipa.

Yanga awali ilipanga kuweka kambi nje ya nchi na China ilikwa inatajwa kwa ajili ya matayarisho ya msimu ujao baada ya kukamilisha zoezi la usajili kwa sasa wapo Morogoro.

"Mpango wetu wa kwenda nje upo na tunachosubiri ni kuona ratiba ya Caf itakapotoka tujue tutacheza na timu gani ndipo taamue wapi tunakwenda kuweka kambi.

"Lengo kubwa ni kwenda kuweka kambi nchi itakayokuwa na hali ya hewa na nchi tutakazopangiwa na Caf baada ya droo kuchezeshwa," amesema.

5 COMMENTS:

  1. Lazima nasi tufanye kama walivofanya watani WA jadi tusikubali kubaki nyuma. Muhimu kuzungusha bakuli bana

    ReplyDelete
  2. Mkipangwa na timu mojawapo ya , afrca kusini , afrika kaskazini na africa magharibi , wataweka kambi wapi ili waendane na hali ya hewa . Hii ni daganya toto , mashindano ya makundi kama unataka uzoee hali ya hewa kama fedha inaruhusu unaenda siku tatu kabla ya mechi , full stop.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic