July 29, 2019



KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa beki wa kikosi hicho Kelvin Yondan hawezi kugoma kama ambavyo inadaiwa hivyo atajiunga ndani ya kikosi hicho muda wowote.


Kelvin Yondani ni mchezaji pia wa timu ya Taifa ni miongoni mwa wachezaji ambao hawajijiunga na timu kambini Morogoro kwa madai ya kuigomea Yanga kushinikiza kulipwa stahiki zao.

Wachezaji wengine ambao hawajajiunga na kambi ni pamoja na Juma Abdul na Andrew Vincet 'Dante'.

Zahera amesema: "Yondani hawezi kugoma ndani ya Yanga kwani ninachojua mimi yeye alipewa likizo na anatumikia pia timu ya Taifa hivyo baada ya majukumu yake atarejea ndani ya kikosi cha Yanga,"amesema.

Zahera ameshawasili kambini Morogoro na jana alishuhudia mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Mawenzi Market uwanja wa Jamhuri na waliibuka kidedea kwa bao 1-0.

3 COMMENTS:

  1. Hamna anayeweza kumfanya lolote Yondani. Kila mtu anajua kagoma lakini Juma Abdul na Vincent Chifupe ndio wametolewa kafara.

    ReplyDelete
  2. Anataka kulazimisha nini?Jamaa kasema kweli.Sisi Yanga Tuna double standard kuhusu suala la wachezaji. Wachezaji wageni wamelipwa kila kitu chao. Yondani ameshindwa kuripoti kwa kuwa na matatizo I assume lakini kambi ya timu ya taifa waliripoti siku hiyo hiyo aliyeitwa.Smell the coffee .Tuzibe sasa Ida kabla hatujalazimika kuziba ukuta.Ligi ndefu hii yasije yakajirudia ya msimu uliopita.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic