July 10, 2019



ALEXIS Sanchez alikubali kusaini kandarasi mpya ndani ya klabu ya Arsenal muda mfupi kabla ya kusaini ndani ya Manchester United kwa mujibu wa mtu aliyekuwa anahusika na mkataba wake Dick Law.
Raia huyo wa Chile alifunga dili lake ndani ya Arsenal na kukubali kuingia ndani ya dili jipya na Arsenal muda mfupi kabla ya mkataba wake kumeguka mwaka 2016 kabla ya kubadili maamuzi.
Ghafla alikubali kuingia kwenye dili la kubadilishana timu na mchezaji Henrikh Mkhitaryan ambaye alijiunga na Arsenal kabla ya yeye kusaini Manchester United muda ambao mkataba wake ulikuwa umebaki miezi sita, Januari 2018.
"Tulikuwa na dili, ilikuwa mwezi Desemba na bado tulikuwa kwenye mazungumzo na wakala wake (Fernarndo Felicevich) kwa muda wote huo tangu mwaka 2016, nilimfuata mpaka Santiago ili kukamilisha dili.
"Niliongea pia na mchezaji kwenye simu alikubali hata wakala wake pia, ila nilishangaa muda ulivyobadilika naye alibadili maamuzi bila sababu yoyote ile," amesema.
Sanchez kwa sasa bado hajapata timu mpya kutokana na dau ambalo United wamelitaja huku timu nyingi zikiwa na hofu ya kumlipa mshahara mkubwa nyota huyo ambaye hajawa na msimu bora ndani ya United.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic