NYOTA wa
timu ya Yanga ambao walikuwa na timu ya Taifa ya Tanzania iliyokuwa ikishiriki
michuano ya Afcon, wanatarajia kujiunga kambini na timu ya Yanga kesho baada ya
kumaliza mapumziko ya siku 14.
Kelvin Yondan,
Ally Mton ‘Sonso’, Feisal Salum walikuwa na timu ya Taifa iliyoshiriki michuano
ya Afcon nchini Misri na kutolewa hatua ya awali bila kuambulia hata pointi
moja.
Kaimu Mtendaji wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa wachezaji
ambao hawakuwa na majukumu ya Taifa wote wamewasili kambini kwa ajili ya
maadalizi ya msimu ujao.
“Tayari
wachezaji wote wamewasili kambini mkoani Morogoro, ambapo maandalizi yetu
yanafanyika uwanja wa Jamhuri hivyo ni muda mzuri kujiaanda kwa ajili ya msimu
ujao.
“Wale ambao
walikuwa na timu ya Taifa pamoja wataunganisha moja kwa moja kambini Morogoro
kwa ajili ya kujiunga na timu ambayo tayari imeanza maandalizi ya msimu ujao,”
amesema Ten.
0 COMMENTS:
Post a Comment