IMEELEZWA kuwa kwa sasa Paul Pogba anafanya visa ndani ya timu yake ya Manchester United kushinikiza asepe.
Pogba hana furaha ndani ya United na ameshaweka nia yake ya kutimka ndani ya kikosi hicho ambacho kwa sasa kimeweka kambi kwa ajili ya msimu ujao.
Pogba alizinguana na mchezaji mwenzake Jesse Lingard nchini Australia kwenye video ambayo ilisambaa mtandaoni.
Beki wa United, Victor Lindelof ameoneka akimzuia Pogba asirejee nyuma kumfuata Lingard ambaye alionekana akiongea.
Pogba anawindwa na Real Madrid pamoja na klabu yake ya zamani ya Juventus.
0 COMMENTS:
Post a Comment