July 29, 2019

MBRAZIL anayekipiga Simba ambaye ni kiraka anacheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji Gerson Vieira amesema kuwa ni furaha kuwa ndani ya Simba kwa sasa.

Vieira  amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya kikosi cha Simba kwenye usajili wa dirisha kubwa akitokea timu ya ATK FC ya India kwa sasa yupo na timu nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Mbrazil huyo amesema :"Wachezaji wenzangu walinipokea vizuri jambo linalonipa furaha na ninafurahi kuwandani ya Simba.

"Tupo na Kocha mwenye uwezo mkubwa hivyo tunaamini tutafanya makubwa pia na kila mmoja yupo vizuri, na tuna kocha mwenye uwezo mkubwa," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Lakini hiyo picha mliyotumia sio ya Vieira.

    ReplyDelete
  2. Mara nyingi kichwa cha maneno hakikubaliani hata kidogo na kile kiandikwacho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic