July 29, 2019



NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul kwa sasa inaelezwa yupo kwenye mgogoro na mabosi wake hao  kutokana na madai yake ya stahiki zake tayari Polisi Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu, Seleman Matola inampigia hesabu.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa tayari mazungumzo ya awali yamefanyika na Polisi Tanzania wanajitahidi kukimbizana na muda kabla ya dirisha kufungwa.

“Dirisha la usajili linafungwa Julai 31 hivyo uongozi wa Polisi Tanzania unapambana kukamilisha dili la Abdul atue ndani ya kikosi,” kilieleza chanzo hicho.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa bado hajapata taarifa kamili kuhusu mchezaji huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic