Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa wachezaji wameanza kambi mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
"Wachezaji wa Yanga kwa sasa wameingia kambi ambayo inafanyika Morogoro na ni maalumu kwa ajili ya kuandaa kikosi bora kitakacholeta ushindani msimu ujao," amesema.
Yanga msimu uliopita walimaliza Ligi Kuu Bara wakiwa nafasi ya pili ambayo imewapa tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya Simba kufanya vema michuano hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment