July 31, 2019


CRESCENTIUS Magori, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa kwa mwaka huu Simba hawatatoa hata shilingi mfukoni kununua vifaa vya mpira kutokana na dili nono walilosaini na kampuni ya UHL Sport.

Magori amesema:-"Kampuni ya UHL Sport Dubai imeshinda tenda ya kutengeneza jezi ya klabu ya Simba kwa msimu wa miaka miwili.

"Ni mkataba mrefu na wenye faida kuliko mkataba wowote ambao Simba imewahi kuingia.

"Hatutatoa pesa mfukoni, mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya milioni 600, kila mwaka ni milioni 300 vifaa vya thamani ya milioni 200 kwa mwaka mzima, vifaa vya mazoezi, mpira na kila kitu kamili," amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic