STRAIKA MPYA YANGA AWACHIMBA MKWARA WABRAZIL SIMBA AKIWA KWAO RWANDA
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amesikia taarifa za usajili wa mabeki wapya wa Kibrazili wa Simba na kutamka kuwa hao ndio anaowataka.
Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu Simba itangaze usajili wa wachezaji watatu kutoka Brazil, kati ya hao wawili mabeki ambao ni Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga Vieira na mshambuliaji, Wilker Henrique da Silva.
Bigirimana ni kati ya wachezaji wapya 13 waliosajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao katika kukiimarisha kikosi chao kinachojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara.
Akizungumza kutoka kwao Rwanda mara baada ya kumvisha pete ya uchumba mchumba wake nyumbani kwao jijini Kigali, Bigirimana alisema kuwa ujio wa Wabrazili hao hautamfanya aiogope Simba mara watakapokutana kwenye ‘derby’.
Bigirimana alisema, siku zote anafurahia kukutana na mabeki wazuri kwa ajili ya kumpa changamoto, hivyo kwake hana hofu ya Wabrazili huku akitamba kujipanga vema kwa ajili ya ushindani.
“Nipo nyumbani Kigali hivi sasa nikiendelea na mazoezi ya binafsi ya gym na ndani ya uwanja katika kujiweka fiti kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
“Nimepanga kuja huko Tanzania kuanzia wiki ijayo (hii) kwa ajili ya kujiunga na kambi ya pamoja ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi na michuano ya kimataifa.
“Nimepata taarifa za Simba ambao ndio wapinzani wetu, wamesajili mabeki Wabrazili, nikwambie tu mimi binafsi siwahofii kabisa na hakuna atakayenizuia nikiamua jambo langu, hivyo wajiandae,” alisema Bigirimana.
Haya tutaona siku zinakaribia
ReplyDelete